1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

RSF yafanya mashambulizi ya droni katika mji mkuu Khartoum

9 Septemba 2025

Wanamgambo wa kikosi cha RSF wamefanya mashambulizi kadhaa ya droni yaliyolenga miundombinu muhimu na maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Sudan katika mji mkuu wa Khartoum.

Sudan Port | Sudan 2025 | RSF
Moshi ukifuka kufuatia shambulio la droni katika eneo la Port SudanPicha: AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa mashahidi, mashambulizi hayo yalilenga kituo cha umeme, kiwanda cha silaha na kiwanda cha kusafisha mafuta karibu na Khartoum.

Ripoti kutoka chanzo cha kijeshi imeeleza kwamba kambi ya jeshi la anga pia imelengwa.

RSF ilithibitisha baadaye kuwa walifanya mashambulizi ya anga "yenye usahihi na mafanikio" katika mji mkuu Khartoum na maeneo mengine, wakieleza kuwa ni sehemu ya operesheni zao dhidi ya serikali inayoungwa mkono na jeshi.

Wanamgambo wa RSF wamekuwa vitani na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023, na walitangaza kuunda serikali pinzani katika maeneo wanayoyashikilia.

Mashambulizi hayo ya leo yametokea miezi kadhaa baada ya jeshi la Sudan kuchukua tena udhibiti wa Khartoum mnamo mwezi Machi, na kutangaza mpango wa ujenzi mpya wa mji mkuu huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW