1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

RSF yashambulia mji mkuu wa Sudan kwa siku ya tatu

23 Oktoba 2025

Wanamgambo wa Sudan RSF wameushambulia mji mkuu, Khartoum na uwanja wake mkuu wa ndege kwa kutumia droni.

Wanamgambo wa RSF nchini Sudan
Wanamgambo wa RSF nchini SudanPicha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Kwa siku ya tatu sasa, RSF imekuwa ikiulenga mji huo kwa mashambulizi.

Mashambulizi ya Alhamisi yamejiri siku moja tu baada ya ndege ya kwanza ya abiria kutua katika mji huo baada ya miaka miwili.

Maafisa wa jeshi la Sudan wamesema hayo huku afisa ambaye hakutaka kutambulishwa akisema walidungua droni hizo na hazikusababisha uharibifu.

Mashambulizi ya RSF yamefanyika wakati kundi hilo likiendeleza shinikizo dhidi ya jeshi la taifa huku mkwamo wa kupata ufumbuzi wa mzozo huo ukiendelea.

Mzozo wa Sudan ulianza mwaka 2023 kufuatia mvutano ulioibuka kati ya jeshi la taifa na kikosi cha RSF ambacho awali kilikuwa sehemu ya jeshi.