RSF yashambulia mji wa Merowe, Kaskazini mwa Sudan
13 Novemba 2025
Taarifa ya jeshi la Sudan imesema droni hizo zimevurumishwa katika makao makuu ya jeshi, uwanja wa ndege na bwawa la Merowe, ikisisitiza kwamba imefanikiwa kuzuwia mashambulizi hayo iliyodai yamefanywa na kundi hilo la RSF.
Huku hayo yakijiri mawaziri wa nchi za nje kutoka mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda duniani G7, wamekosoa vurugu zinazoendelea hukowakisema mapigano kati ya jeshi la taifa hilo na wanamgambo wa RSF, yamesababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu duniani. Marco Rubio waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amesema kundi hilo lina wasiwasi kuhusu visa vya unyanyasaji wa kingono vinavyoendelea katikati ya vita hivyo vilivyodumu kwa takriban miaka miwili.
Katika mgogoro huo wa sudan, pande zote mbili, Jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF, wameshutumiwa na Umoja wa Mataifa kutekeleza ukatili dhidi ya raia katika vita hivyo.