1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubani wa Marekani aliyetoweka Iran aokolewa

5 Aprili 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema rubani wa Marekani aliyetoweka baada ya Iran kudungua ndege ya kivita ya Marekani amepatikana katika operesheni ya uokoaji iliyohusisha ndege kadhaa za kivita.

Marekani Washington D.C. 2026 | Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/dpa/picture alliance

Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social mapema leo, Trump amesema rubani huyo alijificha katika eneo la milima la Iran.

Rubani huyo alikuwa ametoweka tangu siku ya Ijumaa baada ya Iran kudungua ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15E.

Wakati huohuo, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC) kimesema leo kuwa ndege kadhaa ziliharibiwa wakati wa operesheni ya Marekani ya kumtafuta rubani wake nchini Iran. Haya ni kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim.

Mapema leo, jeshi la Iran pia limesema limedungua droni ya Israel kusini mwa mkoa wa Isfahan ilipoangushwa ndege ya Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW