1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruben Amorim atangazwa kocha mpya wa Manchester United

1 Novemba 2024

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye alishinda mataji mawili ya ligi kuu ya Ureno, Primeira Liga akiwa na Sporting Lisbon, amesaini hadi mwaka wa 2027 na ataanza majukumu yake rasmi Novemba 11.

Kocha Ruben Amorim
Kocha Ruben AmorimPicha: Joao Rico/DeFodi Images/picture alliance

Ruben Amorim ametangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United, kuchukua mikoba ya Erik ten Hag. Mreno huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye alishinda mataji mawili ya ligi kuu ya Ureno, Primeira Liga akiwa na Sporting Lisbon, amesaini hadi mwaka wa 2027 na ataanza majukumu yake rasmi Novemba 11.

Manchester United imemuelezea Amorim kuwa mmoja wa makocha chipukizi na wenye kusisimua sana katika kandanda la Ulaya. Ruud van Nistelrooy ataendelea kushika usukani wa timu hadi Amorim atakapowasili Old Trafford wakati wa kipindi cha mapumziko ya ligi mwezi Novemba. Mechi ya kwanza ya Amorim itakuwa dhidi ya Ipswich Novemba 24.Manchester United yaahidi kufanya makubwa zaidi msimu ujao

United ilimtimua Ten Hag Jumatatu wiki hii baada ya kichapo cha 2 -1 dhidi ya West Ham kilichowaacha wakiwa katika nafasi ya 14 kwenye Premier League. Wameshinda mechi tatu tu kati ya nane za mwisho. Amorim ni kocha wa tano kuandikwa kazi na Manchester United tangu Sir Alex Ferguson alipoondoka mwaka wa 2013.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW