1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubiales atakiwa kuomba msamaha kwa kumbusu Hermoso

21 Agosti 2023

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Uhispania amekosolewa na mawaziri wa serikali nchini humo kwa kumpiga busu la mdomoni mchezaji Jenni Hermoso wakati wa sherehe za ushindi wa Kombe lao la Dunia.

FIFA Kandanda la Wanawake Kombe la Dunia I Luis Rubiales amkumbatia Hermoso
Luis Rubiales akimkumbatia Jenny HermosoPicha: Noe Llamas/Sports Press Photo/IMAGO

Katika ukanda wa video uliochapishwa na vyombo kadhaa vya habari vya Uhispania kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Hermoso alisikika akiwaambia wachezaji wenzake kwamba hakufurahia kitendo hicho.

Ila baadae katika mahojiano Hermoso alisema, hilo halistahili kuwa jambo linalozua gumzo na kutilia kiwingu ushindi wao wa kihistoria kwani, ni jambo lililofanyika ghafla tu kutokana na furaha iliyokuwa imetanda.

Jenny Hermoso akipambana na Lucy Bronze wa EnglandPicha: William West/AFP/Getty Images

Mchezaji huyo amesema rais wa shirikisho la kandanda Luis Rubiales anaheshimiana pakubwa na kila mchezaji na hawajawahi kukoseana heshima.

Chanzo: DPAE/APE/Reuters

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW