SiasaAsia
Rubio apigia debe nishati ya Marekani nchini India
23 Mei 2026
Matangazo
Afisi ya Rubio, imesema amesisitiza kuwa Marekani haitairuhusu Iran kushikilia mateka soko la nishati la dunia.
Mgogoro wa nishati uliosababishwa na vita vya Iran umerudisha nyuma juhudi za Marekani za kuondoa utegemezi wa India kwa mafuta ya Urusi.
Wakati huo huo, Modi akikosa kuitaja moja kwa moja Iran katika mkutano huo wa leo, alisisitiza uungaji mkono wa India kwa juhudi za amani na akatoa wito wa utatuzi wa migogoro wa amani kwa njia ya mazungumzo na diplomasia. Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya India.
Huku hayo yakijiri, balozi wa Marekani nchini India Sergio Gor, amesema Rubio alitoa mualiko kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kwa Modi kutembelea ikulu ya White House katika siku zijazo.