Rubio kukutana na Netanyahu Februari 28
19 Februari 2026
Matangazo
Afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina amesema Rubio ataelekea Israel Februari 28 kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Netanyahu ambaye alifanya ziara Washington wiki iliyopita kwa mazungumzo na Rais Donald Trump, kwa muda amekuwa akitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya Iran na Juni mwaka jana aliamrisha kampeni kubwa ya kuishambulia Tehran kwa mabomu.
Trump aliishia kujiunga na kampeni hiyo ambapo aliamrisha kushambuliwa kwa vinu vya nyuklia vya Iran.
Mnamo juzi Jumanne, Trump aliwatuma wajumbe wake kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbas Arraghchi huko Geneva, Uswisi.