Rubio ziarani Israel wakati mashambulizi yanaongezeka Gaza
15 Septemba 2025
Matangazo
Israel imesema inapanga kuukamata kikamilifu mji wa Gaza, ambao ndio mkubwa zaidi kwenye ardhi hiyo ndogo ya Wapalestina.
Mashambulizi ya Israelyamefanyika wakati Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio amewasili nchini humo kwa mazungumzo kuhusu hatma ya vita vinavyoendelea.
Rubio amesema Washington inataka kuzungumza kuhusu mateka wanaoshikiliwa Gaza pamoja na hatua za kuujenga upya ukanda huo.
Matumaini ya kupatikana makubaliano ya kusitisha vita yanazidi kufifia hasa baada ya Israel kuwashambulia kwa makombora viongozi wa kundi la Hamas walipokuwa wakikutana mjini Doha, Qatar wiki iliyopita.
Shambulizi hilo limesababisha msuguano mkubwa kati ya Qatar na Israel mataifa ambayo ni washirika wa karibu wa Marekani.