Rudi Völler arefusha mkataba DFB
8 Aprili 2024Völler, 63, mshambuliaji na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani alichukua kazi hii mpya iliyoundwa baada ya Ujerumani kuondolewa katika Kombe la Dunia la 2022 hatua ya makundi, kama sehemu ya kikosi kazi cha DFB kinachounda mabadiliko.
Timu ya taifa inayonolewa na Julian Nagelsmann sasa imeanza kuimarika baada ya kipindi kigumu, na Völler amehusishwa moja kwa moja na mabadiliko hayo.
"Pamoja na uzoefu wake wote, Rudi Völler ni muhimu na mshauri wangu na pia kwa makocha na wachezaji. Ana ushawishi chanya kwa timu ya taifa," alisema Rais wa DFB Bernd Neuendorf katika taarifa.
"Baada ya kipindi kigumu hivi karibuni, kuna mengi ya shauku kwa timu ya taifa tena. Mbali na kazi bora ya Julian Nagelsmann na timu yake, hii pia ni juhudi ya Rudi Völler." aliongeza Neuendorf.
Matokeo chanya
Ujerumani ilirejea katika fomu yake mnamo Machi katika mechi za kirafiki na ushindi dhidi ya Ufaransa na Uholanzi, na DFB imesema ingependa kuongeza pia mkataba wa Nagelsmann ambao utaendelea hadi michuano ya Euro.
Völler alisema "Katika kipindi cha miezi 14 iliyopita ya kazi yangu, nimetambua
kwamba nimekua nikipenda zaidi na zaidi jukumu langu la uwajibikaji katika
DFB kila siku."
"Kama mkurugenzi wa timu ya taifa , ningependa kutumia uzoefu wangu, nataka kuchukua jukumu katika kuhakikisha kuwa timu bora ya taifa ya soka ya Ujerumani imefanikiwa tena, lakini pia zaidi ya mafanikio ya nyumbani majira ya joto katika Michuano ya Ulaya.
Mustakabali wa Nagelmann
Kocha Nagelsmann amesema angependa hatma yake iamuliwe kabla ya
mashindano ya EURO, na anaweza kuendelea katika usukani wa timu ya taifa Ujerumani au kurudi kwenye ukocha wa klabu.
"Pia tunatarajia kuongeza mkataba wake [Völler] kutuma ishara chanya
kwa kocha wa taifa Julian Nagelsmann, ambaye pia tunapenda kufanya kazi naye kwa muda mrefu," mkurugenzi mkuu wa DFB Andreas Rettig alisema.
Völler aliichezea Ujerumani mara 90, akishinda Kombe la Dunia mwaka 1990 na
akicheza fainali za Kombe la Dunia 1986 na Euro 1992.
Alikuwa kocha wa Ujerumani na alitinga fainali ya Kombe la Dunia 2002 wakati wa uongozi wake 2000-2004, na alikuwa kocha wa muda kwa mechi moja mwaka jana kabla Nagelsmann kuchukua jukumu.
Kabla ya kibarua cha DFB alikuwa mkurugenzi wa michezo kwa muda mrefu
na mkurugenzi mkuu wa michezo katika klabu ya Bundesliga Bayer Leverkusen hadi 2022.