1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruediger: Ufaransa wakali kwenye karatasi tu

Josephat Charo
13 Juni 2021

Beki wa Ujerumani Antonio Ruediger anakiri haonekani kama mchezaji aliyefikia kiwango cha kimataifa lakini anasema sifa hizo hazina umuhimu mkubwa sana kuelekea mechi yao ya ufunguzi na mabingwa wa dunia Ufaransa.

Deutschland - Frankreich Antonio Rüdiger
Picha: picture-alliance/Revierfoto

Beki wa Ujerumani Antonio Ruediger anakiri haonekani kama mchezaji aliyefikia kiwango cha kimataifa lakini anasema sifa hizo hazina umuhimu mkubwa sana kuelekea mechi yao ya ufunguzi ya mashindano ya EURO 2020 na mabingwa wa dunia Ufaransa.

Ruediger alishinda kombe la mabingwa wa Ulaya na klabu ya Chelsea mwishoni mwa mwezi Mei na anaonekana yuko tayari kuanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaft dhidi ya Ufaransa katika kundi F siku ya Jumanne mjini Munich.

"Ufaransa inaonekana kuwa na nguvu zaidi, lakini hiyo ni kwenye karatasi tu," aliuambaia mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili. (13.06.2021)

"Wanaweza kupigiwa upatu kuwa watashinda kombe lakini mimi sijali, bila shaka wana washambuliaji wazuri. Tunahitaji kufanya kazi ya ziada na tuoneshe uwezo wetu. Tuko tayari."

Ruediger, mwenye umri wa miaka 28, alihamia klabu ya Chelsea 2017 baada ya kuichezea kwa muda mfupi klabu ya Roma ya Italia alipoihama klabu ya Bundesliga, VfB Stuttgart.

""Ilikuwa muhimu kwa maendeleo yangu kama mchezaji kuondoka Bundesliga, kujithibitisha mwenyewe katika ligi tofauti na kujifunza lugha mpya. Kuwa mchezaji wa kimataifa bado nahitaji kufanya kazi kidogo," alisema.

Ruediger ni miongoni mwa wachezaji watatu wa klabu ya Chelsea katika kikosi cha Ujerumani pamoja na Kai Havertz na Timo Werner. Anatumai yatatokea marudio ya matokeo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika mashindano ya EURO 2020.

"Bila shaka tulimaliza msimu vizuri, kitu kinachoweza kutusaidia hapa."

(dpa)