1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema imezidungua karibu droni 350 za Ukraine

8 Mei 2026

Urusi imesema leo Ijumaa kwamba imezindungua droni zilizorushwa kuelekea Moscow muda mfupi baada ya kuonya kuhusu uwezakano wa shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Ukraine licha ya kutangaza usitishaji mapigano.

Deutschland München 2026 | Volodymyr Zelenskyy spricht auf der Münchner Sicherheitskonferenz
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Picha: Thomas Kienzle/AFP

Urusi imesema leo Ijumaa kwamba imezindungua droni zilizorushwa kuelekea Moscow muda mfupi baada ya kuonya kuhusu uwezakano wa shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Ukraine licha ya kutangaza usitishaji mapigano wa siku mbili kwa ajili ya maadhimisho ya Vita vya Pili vya Dunia.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kwamba vikosi vyake vimezindungua karibu droni 350 za Ukraine zilivurumishwa usiku kucha.

Saa chache kabla ya kuanza kwa usitishaji mapigano wa Urusi, Rais wa UkraineVolodymyr Zelensky aliwaonya washirika wa Urusi kutohudhuria gwaride hilo.

Hapo jana pia, kiongozi huyo aliikosoa Urusi kwa kupendekeza kusitisha mapigano siku ya Mei 8-9 ilihali ilipuuza pendekezo lao la kusitisha mapigano siku ya Mei 6 na badala yake Urusi iliishia kufanya mashambulizi yaliyowaua watu kadhaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW