1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imeonya kile ilichokiita uhasama wa ndege za Marekani

15 Machi 2023

Urusi imeonya dhidi ya kile ilichokiita uhasama wa ndege za Marekani, wakati mivutano ikitokota siku moja baada ya ndege ya kivita ya Urusi kutuhumiwa kwa kugongana na droni ya Marekani katika anga ya Bahari Nyeusi.

Anatoli Antonow | russischer Diplomat
Picha: Sergei Bobylev/TASS/dpa/picture alliance

 

Washington imeilaumu Moscow kwa tukio hilo, ikikiita kitendo cha marubani wake kuwa cha kizembe, lakini Urusi imekanusha kufanya ubaya wowote.

Balozi wa Urusi mjini Washington Anatoly Antonov amesema wanatumai Marekani itajizuia kutoa uvumi zaidi katika vyombo vya habari na kukomesha kurusha ndege karibu na mipaka ya Urusi.

Soma pia:Droni ya Marekani yaanguka baharini, Urusi yaombwa maelezo

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema droni yake ilikuwa kwenye operesheni ya kawaida wakati ilipokatizwa katika njia ya kizembe, isiyo ya mazingira mazuri na isiyokuwa ya kitaalamu.

Urusiilisema ndege hiyo ilikuwa imepoteza muelekeo ghafla.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW