1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni na makombora

10 Februari 2026

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilikuwa imerusha makombora 11 na droni 149 ikiwa ni pamoja na ndege za kivita aina ya Shahed zilizotengenezwa nchini Iran.

Ukraine I Odesa I  2026
Nyumba iliyoharibiwa huko Odesa kufuatia shambulio la droni la UrusiPicha: Nina Liashonok/REUTERS

Maafisa nchini Ukraine wamesema leo kwamba mashambulizi ya droni na makombora ya Urusi nchini humo usiku wa kuamkia leo yamewaua watu wasiopungua wanne.

Waandishi wa habari wa AFP waliokuwepo katika moja ya eneo la shambulio katika mji wa kusini wa Odesa wamesema waliona majengo yaliyoharibiwa na huduma za zimamoto na dharura zikifanya kazi kwa kutumia mwanga wa taa ili kutoa usaidizi kwa waathirika.

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilikuwa imerusha makombora 11 na droni 149 ikiwa ni pamoja na ndege za kivita aina ya Shahed zilizotengenezwa nchini Iran.

Jeshi hilo limeongeza kwamba lilifanikiwa kuzidungua droni mia moja na makombora kadhaa. Vita hivyo kati ya Urusi na Ukraine vyenye karibu miaka minne bado vimeendelea kuchukua sura mpya kila wakati licha ya juhudi mbalimbali za kuvimalizia vita hivyo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW