1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto afungua ofisi sanjari ya chama cha Jubilee

19 Juni 2020

Naibu rais wa Kenya William Ruto amefungua uwanja mpya wa mapambano na Rais Uhuru Kenyatta katika kuwania udhibiti wa chama cha Jubilee, kwa kuzindua ofisi mpya alioipa jina la Jubilee Asili, yenye makao yake Nairobi.

Kenia William Ruto
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Curtis

Ruto alifungua ofisi hiyo sanjari siku ya Alhamisi iliyopewa jina la Kituo asili cha Jubilee. Kwa kawaida vyama vinyvojitenga na vingine nchini kenya huchukuwa kiambishi tamati cha "Asili". Ofisi hiyo iko Barabara ya Makindu katika eneo la Kilimani mjini Nairobi.

Kwenye anuani hiyo mpya, naibu wa rais Ruto aliwaalika wabunge 20 wa chama cha Jubilee, wakiwemo wale walioondolewa kwenye kamati za bunge na uongozini kwa hatua yao ya kuunga mkono kampeni za urais za naibu huyo wa rais.

Seneta machachari wa Elgeyo-Marakwet Kipchumba Murkomen, alieondolewa kwenye wadhifa wa kiongozi wa walio wengi kwenye bunge la seneti, alisema wameamua kufungua ofisi mpya za chama ili kuweza kuendesha mikutano. Alidai walikataliwa kutumia ofisi za makao makuu ya chama cha Jubilee zilizoko Pangani, barabara ya Thika.

Murkome alithibitisha kwamba mkutano wao na naibu wa rais kuwafariji wale waliolengwa na timuatimua ya rasi Kenyatta ulifanyika siku ya Alhamisi kwenye ofisi hiyo mpya.

"Tulikuwa na mkutano na naibu rais kweyne Kituo cha Jubilee Asili. Ni kituo cha wanachama wote, siyo sanjari. Ni kituo cha chama cha wanachama wa chama cha Jubilee wanaoamini katika dhana ya mwanzo kabisaa ya chama, ikiwemo utekelezaji wa ahadi tuliotoa kwa watu," alisema Murkomeni.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ruto Emmanuel Talam alithibitisha kwamba mkutano huo ulifanyika, na uliitihwa kuwaambia kwamba wana wajibu wa kutekeleza ilani ya chama cha Jubilee iliyokiingiza madarakani mwaka 2013 na 2017.

Keynatta na Ruto wakati waliunda muungano wa Jubilee kabla ya uchaguzi wa 2013.Picha: picture alliance/AP Photo

Sote pamoja

Katika ujumbe wa Twitter, Ruto alisema: "Nilipata chakula cha mchana na wabunge wa Jubilee ambao hivi karibuni walikabidhiwa majukumu mengine ndani ya chama. Nimewashukuru kwa kazi ya kipekee kwa chama na taifa. Nimewahimiza kuendelea kwenye ajenda ya mabadiliko sasa na wakati ujao. Sote pamoja."

Kundi hilo la Tangatanga lilikutana kwenye ofisi mpya siku moja baada ya kambi ya Rais Kenyatta kuwaalika Kalonzo Musyoka na gavana wa zamani Isaac Ruto wa Chama cha Mashinani, ambao vyama vyao vilisaini makubaliano ya ushirikiano kwenye makao makuu ya chama cha Jubilee. Hafla hiyo ilihudhuriwa na katibu mkuu wa Jubilee Rapahael Tuju na makamu mwenyekiti David Mirathe.

Mkutano huo wa Ruto ulikuja siku moja baada ya spika wa bunge la taifa Justin Muturi kutangaza rasmi hatua dhidi ya wabunge walioondolewa kwenye nafasi zao.

Murkomen, mhanga wa kwanza wa timuatimua ndani ya Jubilee, pamoja na Seneta wa Nakuru Sudan Kihika, alietimuliwa kama mnadhimu wa walio wengi kwenye baraza la seneti, alisema kituo cha jubilee asili kimefadhaliwa na wanachama waliohisi kwamba ktik katika miaka mitatu iliyopita wametengwa kwa kunyimwa fursa ya kukutana kwenye makao makuu ya chama.

Seneta Murkomen akasema wakati huo huo kwamba hali hiyo imekuwa na athari hasi kwa michango ya wanachama katika utekelezaji wa ilani yao na ukuaji wa chama. Mbunge wa Belgut Nelson Koech alithibitisha siku ya Alhamisi kuwa kituo hicho ni makaazi mbadala kwa wanchama walioadhibiwa kwa sababu ya mafungamano yao na naibu rais.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW