1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ruto ataka uwekezaji zaidi wa China barani Afrika

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Rais wa Kenya Willium Ruto ameitaka China kuongeza uwekezaji wake katika uchumi wa kidijitali barani Afrika ili kuongeza pato katika bara hilo ambalo kwa sasa linafikia asilimia 4.5.

Afrika-Klimagipfel in Kenia
Rais William Ruto wa Kenya.Picha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Ruto ameyasema hayo katika Kongamano la Miundombinu ya Usafirishaji la China, ambalo lilimalizika siku ya Jumatano (Oktoba 18) na kuongeza kwamba uboreshaji wa miundombinu ungetafsiriwa kuwa "kiwango cha juu cha muunganisho unaohakikisha mabadiliko halisi,"  kufungua demokrasia ya ushirikishwaji na kutoa fursa zisizo na kikomo kwa Afrika.

Soma zaidi: Ruto asema mabadiliko ya tabianchi yanatafuna maendeleo ya Afrika

Kiongozi huyo wa Kenya alikuwa anatafuta kiasi cha dola bilioni 1 kufadhili miradi iliyokwama, na tayari amepata kiasi cha dola bilioni 4.6 katika mikataba ya uwekezaji kutoka kwa makampuni binafsi ya China.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW