1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto atangazwa mshindi wa urais Kenya katikati mwa vurugu

15 Agosti 2022

Mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya amemtagaza naibu wa rais William Ruto kuwa mshindi wa kinyanganyiro kikali cha urais Jumatatu, huku baadhi ya maafisa wa uchaguzii wakijitenga na matokeo, na kuibua hofu ya kutokea vurugu.

Kenia Nairobi | William Ruto gewinnt Präsidentschaftswahl
Picha: TONY KARUMBA/AFP/Getty Images

Akiisifu tume ya uchaguzi kama "mashujaa," Ruto amesema "hakuna kutazama nyuma. Tunaangalia wakati ujao. Tunahitaji ushiriki wa watu wote ili tusonge mbele."

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 55 aliiufanya mgawanyiko wa matabaka nchini Kenya kuwa kiini cha kampeni yake ya kuwa rais wa tano wa Kenya, akiahidi kuwazawadia "wapwaguzi" wenye kipato cha chini huku akikosoa kile alichokiita himaya za kisiasa nchini Kienya.

Soma pia: Matokeo ya IEBC yaonesha Odinga akiongoza, ya Reuters yamuweka Ruto mbele

Hicho kilikuwa kama kidongo kilichoelekezwa kwa mpinzani wakeRaila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta, mtoto wa makamu wa kwanza wa rais na rais wa taifa hilo mtawalia.

Ruto kumrithi Uhuru Kenyatta

01:27

This browser does not support the video element.

Ruto anaeongoza muungano wa Kenya Kwanza, alionekana kuongoza mbele ya Raila ambaye ni kiongozi wa muda mrefu wa upinzani wakati Wakenya wakisubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Dakika chache kabla ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati kutangaza kwamba Ruto ameshinda kura hiyo, naibu wake Juliana Cherera aliviambia vyombo vya habari katika eneo tofauti kwamba yeye pamoja na makamishna wengine watatu wanajitenga na amtokeo hayo.

Soma pia: Ruto: Kutoka mpwaguzi hadi rais aliechaguliwa Kenya

"Hatuwezi kubeba dhima ya matokeo yatakayotangazwa, kwa sababu ya ukosefu wa uwazi katika awamu hii ya mwisho ya uchaguzi mkuu," alisema. Tume ya Uchaguzi inao ma kamishna saba.

Wanadiplomasia na waangalizi wa kimataifa waliondolewa nje ya kituo cha kujumlisha matokeo baada ya kuzuka rabsha. Kabla ya kumtangaza Ruto kuwa mshindi, Chebukati alisema makamishna wawili na mtendaji mkuu wa tume ya uchaguzi walikuwa wamejeruhiwa na walikuwa wanatibiwa.

Chebukati alisema Ruto alishinda asilimia 50.49 ya kura, dhidi ya asilimia 48.5 ya Odinga. Mgombea anaeshinda laazima apate asilimia 50 ya kura ukijumlisha kura moja. Odinga hakuhudhuria hafla ya kutangaza matokeo.

Katikati mwa hofu kwamba madai ya wizi wa kura yanaweza kusababisha matukio ya umwagaji damu yaliofuatia chaguzi za rais mwaka 2007 na 2017, Cherera aliwahimiza wanasiasa kutafuta suluhu ya mizozo kupitia mahakamani.

Wafuasi wa rais mteule William Ruto wakisherehekea ushindi kwenye makao makuu wa chama chake cha UDA mjini Nairobi, baada ya kutangazwa mshindi, Agosti 15, 2022.Picha: Mosa'ab Elshamy/AP/picture alliance

Utaratibu wa kudhibitiana ili kuzuwia matumizi mabaya ya madaraka

Tume ya uchaguzi imeanzisha taratibu nyingi za udhibiti kujaribu kuzuwia migogoro kama iliyosababisha vurugu ambamo watu zaidi ya 1,200 waliuawa kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.

Soma pia: William Ruto atangazwa kuwa rais mteule wa Kenya

Mnamo mwaka 2017, zaidi ya watu 100 waliuawa baada ya mahakama ya juu kabisaa kubatilisha matokeo ya awali kuhusiana na kasoro katika mchakato wa uchaguzi.

Dhamana za serikali ya Kenya zinazohodhiwa na sarafu ya dola zilishuka thamani kwa hadi senti 2.9 kwa dola, kulingana na data za mtandao wa Tradeweb.

Rais ajae atakuwa na kibarua cha kukabiliana na mzozo wa kiuchumi na kijamii katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki, ambako Wakenya maskini wanaopambana na athari za janga la Covid-19 wamekumbwa na kupanda kimataifa kwa bei za chakula na mafuta.

Soma pia: Tuhuma za wizi wa kura zazuwa mashaka uchaguzi Kenya

Ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40 umeathiri vibaya upande wa kaskazini mwa nchi hiyo, na kuwaacha watu milioni 4.1 wakitegemea chakula cha msaada, huku viwango vya deni la taifa vikiongezeka.

Wafuasi wa mgombea wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga wakiandamana na kuchoma matairi katika eneo la Kibera mjini Nairobi, Agosti 15, 2022.Picha: MARCO LONGARI/AFP/Getty Images

Kenyatta, ambaye amehudumu mihula yake mwili inayoruhusiwa kikatiba kama rais, alikosana na Ruto baada ya uchaguzi uliopita na safari hii alimuidhinisha Odinga, katika jaribio lake la tano la kuusaka urais.

Vurugu zashuhudiwa Kisumu

Katika mji wa Kisumu, ambao ni gome ya Odinga magharibi mwa nchi, uitikiaji ulikuwa wa haraka. Watu walianza kuchoma matairi na moshi mweusi ulishuhudiwa ukitanda angani.

Soma pia: Chama cha UDA cha taraji ushawishi mkubwa bungeni Kenya

Katikati mwa kele za "Tunamhitaji Raila sasa hivi!", "Chebukati laazima aondoke!" na "Hakuna Raila hakuna amani!", waednesha pikipiki walipiga honi zao huku watu wengine wakipuliza mavuvuzela na firimbi.

Kwa kulinganisha, hali katika mji wa Eldoret - ambao ni ngome ya Ruto ilikuwa ya furaha na vifijo.

"Tuna furaha sana. Naamini katika kiongozi aliechaguliwa, naiamini IEBC", alisema mkaazi wa Eldoret Kenneth Kibitok, mwenye umri wa miaka 25.

"Yeye anataka kuwainua watu kutoka chini kwenda juu. Watu kutoka chini kabisaa watakuwa juu huko," alisema Kibitok, ambaye alitumia siku nzima kwenye njia ya waenda kwa miguu mjini Eldoret, ambayo ni maarufu kwa Wakenya wanaopedna kujadili siasa.