1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto na Odinga jino kwa jino Kenya

10 Agosti 2022

Matokeo ya awali katika uchaguzi mku wa Kenya yanaonesha kuna mjongeleano wa karibu kati ya wagombea wawili wakuu wanaowania kuchukua nafasi ya rais Uhuru Kenyatta.

Kenia Wahlen Raila Odinga William Ruto
Picha: AFP

Wananchi wa Kenya wanasubiri matokea huku wakifanya ibada ya kufanikisha matokeo ya uchaguzi huo yasije kuliingia taifa hilo katika vurugu.

Uchaguzi huo wa Jumanne unaatazamwa kama jaribio muhimu la hali ya utuluvu kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika eneo la Afrika Mashariki. Chaguzi mbili kubwa zilizopita zilisababisha uvunjifu wa amani kutokana tuhuma za wizi wa kura.

Polisi inamsaka mbuge mtuhumiwa wa mawaji.

Polisi wa Kenya wakiwa kaziniPicha: Billy Mutai/SOPA/ZUMA/picture alliance

Kimsingi zoezi la kupiga kura la jana Jumanne lilikuwa la utulivu ingawa polisi inasema ilikuwa ikimsaka mbunge mmoja aliyempiga risasi na kumuuwa msaidizi wa mpinzani wake nje ya kituo cha kupigia kura.

Wakenya wanasubiri kwa shauku matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa wa amani ijapokuwa ulishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura. Matokeo ya mwanzo yanayotangazwa na televisheni za nchini humo yanaashiria kinyang'anyiro kikali kati ya Naibu Rais William Ruto na Raila Odinga, kiongozi mkongwe wa upinzani ambaye sasa anaungwa mkono na chama tawala.

Wagombea hao wawili wameapa kudumisha amani kufuatia uchaguzi huo wa jana. Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka - IEBC, wanaendelea kuhesabu kura na kuondoa hofu ya kuwepo udanganyifu. Tume hiyo ina hadi Agosti 16 kutangaza matokeo ya mwisho.

Soma zaidi:Kenya: Maafisa wa uchaguzi wakesha wakihesabu kura

Mpaka sasa, kituo kikuu cha kujumlisha matokeo kimepokea zaidi ya asilimia 95 ya fomu za matokeo ya rais zilizowasilishwa kielekroniki kutoka vituo vya kupigia kura kote nchini humo. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati aliwasihi Wakenya kuwa wavumilivu wakati shughuli ya kujumlisha kura ikiendelea.

Chanzo: RTR

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW