1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto asema yupo tayari kukutana na Odinga wakati wowote

27 Julai 2023

Kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali, Rais William Ruto amesema yuko tayari kukutana na kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga wakati wowote atakapomuhitaji.

Kenia Kenianische Aktivisten demonstrieren in Nairobi gegen ein unpopuläres Finanzgesetz
Waandamanaji nchini Kenya wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maishaPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Wakenya waliochoshwa na maandamano wameonyeshwa matumaini ya kusitishwa kwa machafuko ya kisiasa, baada ya Rais William Ruto kusema yuko tayari kukutana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakati wowote.

Kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali, tangu mwanasiasa huyo mkongwe Odinga, kuwataka Wakenya kujitokeza barabarani mwezi Machi, muungano wa Azimio umefanya maandamano ya siku tisa dhidi ya serikali, huku maandamano hayo yakipelekea uporaji mali na makabiliano makali na jeshi la polisi.

Rais Ruto ameelezea nia yake ya kukutana na kiongozi huyo wa upinzani, Odinga kupitia ujumbe aliochapisha katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema "kama ambavyo unajua siku zote ninapatikana, na ninaweza kukutana na wewe ana kwa ana wakati wowote kwa urahisi ukihitaji." 

Rais wa Kenya William RutoPicha: Ihsaan Haffejee/AA/picture alliance

Kufuatia ujumbe huo hakukuwa na jibu la mara moja kutoka kwa Odinga, ambaye amezidi kuwataka Wakenya wajitokeze katika maandamano na mikesha kuipinga serikali, juu ya mauaji ya waandamanaji waliouawa kwenye maandamano hayo.

Odinga ambae alisitisha maandamano mwezi Aprili na Mei baada ya Ruto kukubali mazungumzo, lakini mazungumzo hayo yalivunjika, na maandamano kadhaa yamefanyika mwezi huu. 

Soma pia: Kenya yahitimisha siku ya tatu ya maandamano

Wakenya kadhaa waliambia shirika la habari la AFP kuwa wamechoshwa na usumbufu huo na kuzitaka pande hizo mbili kutafuta "amani." 

Wameeleza kuwa inawawia ugumu kwenda kazini kila kunapokuwa na maandamano kwa sababu ya hofu ya kushambuliwa barabarani na kuibiwa. Huku wakisisitiza kusipofanyika mazungumzo ya amani hali hiyo haitaisha na mateso kwao yataendelea.

Ghasia hizo ambazo pia zimezua hasira miongoni mwa makundi ya kutetea haki za binadamu, huku wanakampeni wakilaani polisi kwa kurusha mabomu ya machozi na kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe. 

Watu 20 wameuawa, kulingana na takwimu rasmi, ingawa Azimio awameeleza kuwa idadi ya waliouawa ni 50. Azimio siku ya Jumatatu ilisema itaandaa "gwaride la mshikamano na mkesha kwa waathiriwa wa ukatili wa polisi." 

Polisi wakiwatawanya waandamanaji mjini KisumuPicha: James Keyi/REUTERS

Muungano huo uliwataka Wakenya wajitokeze kuwasha mishumaa na kuweka maua, ikiwezekana meupe, ili kuwakumbuka na kuwaheshimu waathiriwa.

Odinga, ambaye anasema matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana "yaliporwa" kutoka kwake, ameilaumu serikali kwa upandaji wa gharama ya maisha. Na ameishutumu mamlaka kwa ukatili unaofanywa na polisi ambao amesema haujawahi kutokea.

Soma Zaidi: Zaidi ya watu 300 wakamatwa baada ya kuandamana, Kenya

Huku mashirika ya kutetea haki za binadamu likiwemo Amnesty International yakisema walikuwa na ushahidi wa unyongaji kinyume na sheria. Wizara ya mambo ya ndani imesema madai hayo ya unyongaji bila ya mahakama au uwepo wa matumizi ya nguvu kupita kiasi ni ya uongo na yanalenga kupotosha umma".
  
Odinga ambaye anasema matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana "yaliporwa" kutoka kwake, ameilaumu serikali kwa upandaji wa gharama ya maisha. Na ameishutumu mamlaka kwa ukatili unaofanywa na polisi ambao amesema haujawahi kutokea.

Kiongozi wa muungano wa Azimio Raila OdingaPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Rais Ruto ametoa wito mara kwa mara wa kusitishwa kwa maandamano hayo, na kuapa kukabiliana na dalili zozote za machafuko. Huku maandamano yakiendelea, shauku ya ya maandamano imepungua kasi, huku baadhi ya Wakenya wakipuuza kwa kiasi kikubwa wito wa kufanyika mikutano siku tatu mfululizo. 

Maandamano ya upinzani kufuatia kushindwa kwa Odinga katika uchaguzi wa 2017 yaliendelea hadi alipofikia makubaliano ya kushtukiza na mpinzani wake wa zamani, rais Uhuru Kenyatta, ambayo yanajulikana kama "kupeana mikono".
 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW