1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rutte asema Ulaya imepokea ujumbe wa Trump kuhusu Usalama

4 Mei 2026

Mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Mark Rutte, amesema leo kuwa Ulaya imepata ujumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump wa mafadhaiko kuhusu vita vya Iran na "itachukuwa hatua.''

Armenia Yerevan 2026 |Mkutano
Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO, Mark RuttePicha: Anthony Pizzoferrato/AP Photo/picture alliance

Akizungumza kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Siasa ya Ulaya (EPC) mjini Yerevan, Armenia ambao utatawaliwa na ajenda ya vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, Rutte alikiri kughadhabishwa kwa Marekani kutokana na hatua ya washirika wake wa Ulaya kukataa kujiunga na vita hivyo.

"Kwa ujumla, tumeona kukatishwa tamaa kwa upande wa Marekani kwa hatua za Ulaya kwa kile kinachoendelea nchini Iran na kwa Marekani kujaribu kuhakikisha kuwa dunia iko salama zaidi kwa kuhakikisha kwamba uwezo wa Iran wa nyuklia na makombora ya masafa marefu unaharibiwa. Lakini wakati huo huo, ningependa kusema, Ulaya imesikia ujumbe huo."

Rutte amesema Ulaya inajiimarisha katika kusimamia bara hilo na muungano wa  NATO wakati viongozi mbali mbali wa Ulaya akiwemo Ursula von der Leyen na  rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wakitilia mkazo kwamba Ulaya inapaswa kuiweka hatma mikononi mwao na kuimarisha bajeti zao za usalama na ulinzi.

    

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW