1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Umoja wa Ulaya hauna haja ya kujitenga na Marekani

26 Desemba 2025

Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, ameonesha kutoamini kuwa Umoja wa Ulaya unahitaji kujitenga kabisa na Marekani katika masuala ya ulinzi, licha ya mwelekeo wa sasa wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

USA Washington D.C. 2025 | Wolodymyr Selenskyj und Regierungschefs beim Besuch im Weißen Haus
Wakuu wa serikali wakati wa ziara katika Ikulu ya White House,Washington D.C. 2025. Picha: The Presidential Office of Ukraine/Captital Pictures/picture alliance

Akizungumza na Shirika la Habari la Ujerumani DPA, Rutte amesema Marekani inatarajia Ulaya ichukue jukumu zaidi na itumie fedha zaidi kwa ulinzi. Na kwamba ana uhakika kabisa kuwa Marekani imewekeza kikamilifu katika NATO. Rutte, amesema mkutano wa NATO wa Juni mjini The Hague ulikuwa hatua muhimu, baada ya washirika wote kukubaliana kuongeza matumizi ya ulinzi hadi asilimia 5 ya pato la taifa (GDP) ifikapo mwaka 2035. Aidha alieleza kuwa makubaliano hayo ni moja ya mafanikio makubwa ya sera za kigeni ya Rais wa Marekani Donald Trump, akisisitiza kuwa ahadi hiyo ya wazi ya kuchangia zaidi inaonyesha mshikamano wa muungano huo katika kuimarisha uwezo wa kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW