1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Mshukiwa akiri kuwaua watu 14, waliomuambukiza VVU

21 Septemba 2023

Mshukiwa wa mauaji ya kupanga nchini Rwanda amekiri hii leo mbele ya Mahakama ya Kicukiro mjini Kigali, kuwa na hatia ya kuwaua watu 14, wengi wao wakiwa wanawake na mwanamume mmoja

AIDS in Kamerun
Picha: JOE KLAMAR/AFP/Getty Images

Denis Kazungu, 34, amekiri mashtaka hayo ambayo ni pamoja na mauaji, ubakaji na wizi. 

Kazungu amesema licha ya kutokuwa na ushahidi wowote, kwamba aliwaua watu hao kwa sababu walimwambukiza kwa makusudi Virusi vya UKIMWI.

Hata hivyo majina ya wahanga wa muuaji huyo hayajafahamika vyema. Kazungu hakuwa na wakili na atafikishwa tena Mahakamani Jumanne ijayo.

Lakini mshukiwa huyo ameomba kesi hiyo isiwekwe hadharani ili kuepusha kuzua hamasa kwa watu wengine kufuata nyayo zake.

Polisi wamedai kuwa mshukiwa huyo alikuwa akiwarubuni watu katika migahawa na kuwapeleka hadi nyumbani kwake katika kitongoji cha Busanza mjini Kigali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW