Rwanda, Msumbiji zasaini makubaliano ya 'amani na usalama'
28 Agosti 2025
Makubaliano hayo yamesainiwa mnamo wakati mashambulizi ya wanamgambo nchini Msumbiji yameongezeka huku vikosi vya nchi hizo mbili vikipambana dhidi ya uasi wa muda mrefu wa wanamgambo, kaskazini mwa Msumbiji.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ameyakaribisha makubaliano hayo na kusifia kile alichokitaja kuwa 'uhusiano thabiti' baina ya nchi hizo mbili.
Kulingana na shirika la habari la serikali ya Rwanda RBA, Rais Chapo amesema mkataba huo ni chombo muhimu kwa vikosi vya jeshi la Rwanda vilivyoko Msumbiji.
Hata hivyo, maelezo kamili ya makubaliano hayo hayakuwekwa wazi moja kwa moja.
Hali mbaya ya usalama kaskazini mwa Msumbiji, imesababisha watu wengi kuyakimbia makaazi yao na shughuli za kampuni za kigeni za uchimbaji mafuta na gesi kutatizika katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.