1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda na jimbo la Ujerumani kuimarisha ushirikiano

Sylvanus  Karemera2 Oktoba 2018

Waziri mkuu wa jimbo la Rhineland Palatinate nchini Ujerumani Malu Dreyer amesema uhusiano wa Ujerumani hasa jimbo lake ni wa miaka 38 sasa lakini uhusiano huo sasa wakati umefika upige hatua zaidi .

SPD-Parteitag in Berlin | Malu Dreyer; Ministerpräsidentin Rheinland-Pfalz
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Serikali ya Jimbo la Rhineland Palatinate nchini Ujerumani pamoja na serikali ya Rwanda wamekubaliana kuimarisha uhusiano wao kwenye nyanja mbalimbali. Hayo yanafuatia ziara ya waziri mkuu wa jimbo hilo Malu Dreyer na ujumbe wake nchini Rwanda.

Bibi Malu Dreyer na ujumbe wake wanaendelea kuyazuru maeneo mbalimbali ya uongozi nchini Rwanda huku wakifanya mazungumzo na maafisa wa ngaza zi juu serikalini. Baada ya kuzuru wizara ya serikali za mitaa na bunge Bi Dreyer amesema kwamba uhusiano wa Ujerumani hasa jimbo lake la Rhineland Palatinate ni wa miaka 38 sasa lakini uhusiano huo sasa wakati umefika upige hatua zaidi . Alikuwa akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na spika wa bunge la Rwanda NBi Donatille Mukabarisa

"Mfano mzuri wa jana ambapo tulitembelea maonyesho ya vijana wa pande mbili ambayo yanaoyesha ubunifu wao kwenye nyanja mbalimbali na tunadhani huu ni mfano bora ambao tunaweza kuutumia kubadilishana ujuzi kwa pande zetu mbili na niseme kwamba hii inatupa changamoto zaidi za kubuni ni maeneo gani zaidi tunayoweza kushirikiana hasa kupeana ujuzi."

Wito wa uhusiano kuleta tija kwa serikali kuu

Waziri wa serikali za mitaa nchini Rwanda Franscis Kaboneka naye ametaja umuhimu wa kuwepo na makubaliano zaidi baina ya Rwanda na jimbo hili la Ujerumani kuhusu kupiga hatua zaidi kuliko ilivyo sasa kiasi kwamba hata serikali kuu zipate tija kutokana na uhusiano huu.

Uhusiano wa Ujerumani hasa jimbo la Rhineland Palatinate na Rwanda umedumu kwa miaka 38.Picha: Carl Court/AFP/Getty Images

"Lengo ni kuimarisha uhusiano wetu na ambao utazaa matunda kwa wananchi wa Rwanda na wale wa jimbo la Rhineland Palatinate. Na ndiyo maana tumeamua kuongeza kasi ktk kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuandika ukurasa mpya na tunadhani kwa hatua hii wote tutafaidika."

Wakfu wa kuwasaidia vijana wazinduliwa

Wakati huo huo wakfu wa Guido Westerwelle aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Ujerumani umefunguliwa jijini Kigali ikiwa ni sehemu ya ushirikiano huu wa Rwanda na Jimbo hilo la Ujerumani.

Wakfu huu unalenga kuwasaidia vijana chini ya umri wa miaka 25 wenye miradi ya ujasiliamali hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia.

Ni kituo maalum ambacho vijana wanasema kimekuja wakati muafaka , wakiwa katika  jitihada  za kujikwamua kimaisha. Kijana mmojawapo anasema:

"Itatusaidia maana kama unavyoona hapa tunakutana kama mabinti waliobobea kwenye teknolojia lakini bila mitaji kwa hiyo kuja kwa wakfu huu wa Westewelle utatusaidia kuinukia."

Bi Malu Dreyer na ujumbe wake wanatazamiwa kukutana na Rais Paul Kagame jioni ya leo kwa mazungumzo zaidi.

 

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW