Rwanda: Sherehe za Sikukuu ya walimu duniani
5 Oktoba 2009
Matangazo
Ahadi hiyo imetolewa na wizara ya elimu katika sherehe za kusherehekea siku kuu ya walimu duniani leo, katika sherehe mjini, Kigali. Katika sherehe hizo, walimu sitini walioongoza kwa ufanisi darasani walipewa tuzo zikiwemo kompyuta za laptop, pesa taslimu na vitabu. Juhudi hizi zinalenga kurejesha matumaini katika fani hii ya ualimu, ambao wengi wamekuwa wakiikimbia kwa kuwa haina maslahi kama fani nyingine.
Mwandishi wetu wa Kigali Daniel Gakuba ametuandalia taarifa ifuatayo.
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mpitiaji Munira Muhammad