1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Watu 11 wafa kwa Marburg

4 Oktoba 2024

Mamlaka za Afya nchini Rwanda zimesema homa hatari ya Marburg inayohusisha mgonjwa kuvuja damu imewaua watu 11 wakati juhudi zinafanyika kubaini chanzo la mripuko wa maradhi hayo.

Marburg
Mchoro wa kirusi cha Marburg.Picha: Science Photo Library/IMAGO

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Rwanda imesema hadi sasa visa 36 vya maambukizo vimethibitishwa na wagonjwa 25 wamewekwa karantini. Rwanda ilitangaza mlipuko wa homa ya Marburg mnamo Septemba 26 na kutangaza vifo vya watu 6 siku moja baadaye.  

Mamlaka ziliarifu kwamba visa vya mwanzo viligundulika kutoka kwa wagonjwa waliokuwa hospitali na uchunguzi umeanzishwa kubaini kwa uhakika chimbuko la mripuko huo wa sasa. 

Soma zaidi: BioNTech inapanga kufungua kiwanda chake Afrika

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha juu ya uwezekano wa kusambaa ugonjwa huo duniani kwa sababu mji mkuu wa Rwanda, Kigali ni lango la safari nyingi za kimataifa. 

Mapema wiki hii, watu waliosafiri kutoka Rwanda kuja mji wa Hamburg nchini Ujerumani walithibitika kuwa na maambukizo ya homa ya Marburg na tangu wakati huo wamewekwa karantini.