1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Wengine watano wafa kwa Marburg

2 Oktoba 2024

Watu watano wamekufa nchini Rwanda baada ya kuambukizwa virusi vya Marburg vinavyofanana na Ebola na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 11.

Marburg
Kirusi cha Marburg.Picha: CDC/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, karibu watu 29 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu ulipozuka Septemba 27.

Wizara hiyo ilisema watu 19 miongoni mwao wametengwa na kuendelea kutibiwa kote nchini humo.

Soma zaidi: Sita wafa kwa Marburg Rwanda

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Barani Afrika (CDC) kilisema siku ya Jumanne (Oktoba 1) kwamba wengi wa wagonjwa ni wahudumu wa afya na tayari wamewafuatilia zaidi ya watu 290 waliokaribiana nao.

Virusi vya Marburg husambaa kwa kugusa majimaji ya mgonjwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW