1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yaanza kutumia 'drones' katika vita dhidi ya corona

Sylivanus Karemera/dw Kigali15 Aprili 2020

Nchini Rwanda polisi wameanza kutumia ndege ndogo zisizo na rubani, drone, kuwahamasisha watu mitaani kuheshimu amri ya kubakia nyumbani kama mkakati wa kuzuia kusambaa kwa virusi virusi hivyo,

Drone iliyozinduliwa Rwanda mnamo Oktoba mwaka 2016 kusaidia kupeleka dawa vijijini.
Drone iliyozinduliwa Rwanda mnamo Oktoba mwaka 2016 kusaidia kupeleka dawa vijijini. Picha: Getty Images/AFP/S. Aglietti

Ni ndege ndogo zisizoendeshwa na rubani, yaani drone ambazo serikali ya Rwanda kupitia jeshi la polisi imeanza kuzitumia kusambaza ujumbe katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu kuepuka virus vya Corona. Msemaji wa jeshi la polisi nchini hapa  Polisi John Bosco Kabera anaeleza madhumini ya hatua hiyo.

"Hizi ndege zina kazi mbili za kufanya kwanza kuendelea kuwapa ujumbe wananchi unaowataka wasitoke nje ya nyumba zao au kufanya safariu zisizo za lazima/Lakini pili ni ndege hizi kutoa taarifa ya pale ambao inawezekana wananchi wamejikusanya bila sababu na hivyi kushindwa kuheshimu zile mita baina ya mtu na mtu." Amesema Bosco

Wananchi nao wanasema kwamba licha ya kutakjiwa kusaliamajumbani mwao badokulikuwepo baadhi yao ambao ni kama walikiuka miito hii na mara kadhaa kutoka zao nje.

Ndege zinarushwa kupita ya paa za nyumba katika makazi ya watu huku ujumbe kutoka kwenye kipaza-sauti kilichofungwa kwenye ndege hiyo ndogo kikiwataka watu kusalia nyumbani na kuendelea kuzingatia mawaidha ya kujilinda dhidi ya virus vya corona.

Rwanda tayari inahesabu visa 134 huku watu 49 miongoni mwao wakiwa wameshapona na kurejea nyumbani na 85 wakiendelea kutibiwa hospitali.

'Drones' hizo kutumika kusambaza ujumbe vijijini na maeneo ya mbali kuhusu coronaPicha: Reuters/R. Muharrman

Tangu kilipopatikana kisa cha kwanza cha mtu mwenye virus vya ugonjwa wa covid-19 mapema mwezi wa tatu, Rwanda ilianzisha mikakati ya kuukabili ugonjwa huo. Na tarehe 21 mwezi uliopita serikali ikatangaza zuio la wananchi kusalia majumbani kwa muda wa wiki ambazo zilikuja kuongezwa hadi tarehe 19 mwezi huu wa nne.

Kadri idadi ya wagonjwa Corona ilivyopanda pia, serikali ilichukua jitihada za maksudiikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo mbalimbali vya kupima ugonjwa huu kwa kutumia vifaa vya kisasa. Waziri wa afya Dr Daniel Ngamije amesema kwamba kwa sasa wizara yake ina uwezo wa kuukabili ugonjwa huo.

"Tangu tulipoanza kupima wagonjwa wa corona, hadi sasa tumeshapima watu elfu nane,ambapo tuliwachukua vipimo zaidi ya elfu kumi na moja, tunasema hivi kwa sababu kuna wakati mtu tunampima mara mbili.Na kutokana na juhudi hizi hakuna kifo kilichokwishatokea na wala hakuna mtu aliyeko chumba cha wagonjwa mahtuti ICU." Amesema waziri wa Afya Dkt. Daniel Ngamije

Hata hivyo mkakati wa kuwataka watu kukaa majumbani uliwaathiri kwa kiasi kikubwa idadi kubwaya watu waliotegemea kazi za vibarua kwa ajili ya kujikumu na ndipo serikali ikachukua uamuzi wa kuanza kuwapa vyakula watu hao. Mwezi huu pia serikali ya Rwanda ilitangaza kukata mishahara ya viongozi wakuu serikali kama vile mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa taasisi za serikali.Pesa hii kwa mujibu wa serikali itakwenda kusaidia kuwanunulia vyakula watu waliopoteza jinsi ya kupata chakula kutokana na ajira zao kusimama.