1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaRwanda

Rwanda yaanza majaribio ya kutibu virusi vya Marburg

16 Oktoba 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limesema Rwanda imeanza majaribio ya kwanza duniani ya kutibu ugonjwa unaotokana na virusi vya Marburg, ambao umeua zaidi ya watu kumi na mbili nchini humo.

Rwanda yaanza majaribio ya kwanza ya kutibu virusi vya Marburg
Rwanda yaanza majaribio ya kwanza ya kutibu virusi vya MarburgPicha: DmitriySk/Depositphotos/IMAGO

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba hizo ni habari za kutia moyo kutoka Rwanda huku akipongeza hatua hiyo inayohusisha matumizi ya dawa inayotumiwa pia kutibu Covid-19.

Mripuko wa Marburg ulitangazwa kwa mara ya kwanza nchini Rwanda mwishoni mwa mwezi Septemba huku kampeni ya chanjo ya majaribio ikizinduliwa mapema mwezi huu. Wiki iliyopita, Idara ya afya ya Umoja wa Afrika ilisema kuwa mlipuko huo kwa sasa umedhibitiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW