1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yadai mkoasoaji wake aliyetoweka aliingia Uganda

17 Februari 2022

Polisi ya Rwanda imesema kuwa mtunga mashairi maarufu na pia muimbaji raia wa nchi hiyo Innocent Bahati ambaye alitoweka mwaka mmoja uliopita, amejiunga na kundi la uasi.

Afrika Ruanda Poet Innocent Bahati
Picha: Alex Ngarambe/DW

Bahati mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliweka katika mtandao wa Youtube mashairi yanayoikosoa serikali, alitoweka tarehe 7 Februari mwaka uliopita, hali iliyosababisha hofu miongoni mwa makundi yanayoituhumu serikali ya Rwanda kutovumilia sauti za ukosoaji.

Msemaji wa kitengo cha uchunguzi wa uhalifu cha Rwanda, RIB  Thierry Murangira amesema hapo jana kuwa uchunguzi wao umeonyesha kuwa Bahati mara kadhaa aliwahi kuingia Uganda kupitia njia zisizo rasmi, na alikuwa na mawasiliano na maafisa wa Usalama wa Uganda na watu kutoka makundi yanayoipinga serikali ya mjini Kigali. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW