1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yafikishwa Mahakamani

4 Julai 2005

The Hague:

Rwanda imekanusha leo tuhuma kuwa Wanajeshi wake wanavunja haki za binaadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Imesema kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki haina uwezo wa kuhukumu kesi hiyo. Kongo-Kinshasa imepeleka kesi yake kwenye Mahakama hiyo mwaka 2002 na kuituhumu Rwanda kuwa imekuwa ikitumia nguvu katika ardhi yake kuanzia mwezi wa Agosti mwaka 1998, kuua kiholela, kubaka Wanawake, kuwafunga watu kiholela na uizi wa mara kwa mara. Kongo-Kinshasa imeiomba Mahakama itoe hukumu ya kuwaamuru Wanajeshi wa Rwanda waondoke katika ardhi yake na ilipe fidia. Rwanda imeondoa rasmi Wanajeshi wake mwaka 2002 lakini serikali ya Kinshasa inashikilia kuwa Wanajeshi wa Rwanda bado wangaliko mashariki mwa nchi hiyo, dai ambalo linakanushwa na serikali ya Rwanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW