1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yaikosowa Ubelgiji kutomuidhinisha balozi wake

27 Julai 2023

Rwanda imeelezea kusikitishwa na hatua ya Ubelgiji kukataa kuidhinisha uteuzi wa balozi wake, Vincent Karega, ambaye amewahi kuiwakilishia nchi hiyo nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Ruanda l Präsident Paul Kagame
Picha: Dan Kitwood/POOLAFP

Balozi Karega alifukuzwa na serikali ya Kinshasa mwezi Oktoba 2022 kutokana na mvutano kati ya nchi hizo mbili, na ndipo alipoteuliwa kuwa balozi nchini Ubelgiji.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, amesema inasikitisha sana kuona kwamba serikali ya Ubelgiji inaonekana imekubali shinikizo la Kongo na propaganda kutoka kwa mashirika na wanaharakati wanaoipinga.

Athari za kufukuzwa kwa balozi wa Rwanda nchini DRC ni zipi?

This browser does not support the audio element.

"Hatua hii haifai kwa uhusiano wa mataifa haya mawili," alisema msemaji huyo wa serikali ya Rwanda.

Kongo ilimfukuza Karega ikiishutumu Rwanda kwa kuliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Rwanda.

Wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji bado haijazungumzia suala hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW