SiasaRwanda
Rwanda yamuachia huru Paul Rusesabagina
25 Machi 2023Matangazo
Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo jana aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa amri hiyo ya rais ya kumuachilia Rusesabagina ilitolewa baada ya ombi lililotolewa kwa niaba ya Rusesabagina.
Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, Rusesabagina, aliyesifika kwa kuokoa maisha ya watu 1,200 katika hoteli aliyoisimamia wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 baada ya kuachiliwa alikwenda moja kwa moja hadi kwenye makazi ya balozi wa Qatar mjini Kigali.
Anatarajiwa kuondoka Rwanda siku chache zijazo. Rais wa Marekani Joe Biden, ameipongeza hatua hiyo ya kuachiliwa Rusesabagina na kuzishukuru serikali za Rwanda na Qatar na maafisa wa Marekani waliohusika kufanikisha matokeo hayo aliyoyaita ya furaha.