1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yapokea shenena yake ya chanjo ya corona

3 Machi 2021

Rwanda imepokea awamu ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya corona. Jumla ya chanjo 240,000 za AstraZeneca/Oxford zimetumwa kwa ajili ya kuwachanja watu walioko kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.

Südafrika Cornavirus Ankunft Impfstoff
Picha: via REUTERS

Zoezi la kutoa chanjo litaanza kesho mjini Kigali ambako maambukizi ya virusi hivyo yalitajwa kuwa katika kiwango cha juu.

Shehena ya chanjo hizi imewasili mjini Kigali mapema Jumatano huu ukiwa ndiyo mwanzo wa Rwanda kuanza kuzipokea chanjo za ugonjwa wa COVID-19 kama ambavyo serikali imekuwa ikisema.

Awamu nyingine ambayo itakuwa na chanjo aina ya Pfizer inatarajiwa kuwasili Rwanda baadaye jioni. Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni mchanganyiko kuhusu chanjo hii iliyowasili mapema leo mjini Kigali.

Baadhi ya wananchi wana wasiwasi kuhusu ubora wa chanjo

''Kwangu mimi naweza kusema kwamba hii ni ishara ya matumaini kwa sababu tumekuwa kwenye hali ya mkanganyiko kwa muda sasa, na kwa hali hii basi kuna matumaini kwamba huenda tukarejea katika hali ya kawaida,'' alisema mmoja wao.

Chanjo ya AstrazenecaPicha: Valentina Petrova/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo baadhi ya wananchi wana wasiwasi kuhusu ubora wa chanjo hizi. Nimemuuliza mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, kama yuko tayari kupokea chanjo yake.

''Nadhani hilo ni swali zito, utayari wangu kupokea chanjo utategemea aina ya chanjo, kama ni chanjo ya Pfizer hiyo itakuwa habari njema, lakini kama ni chanjo ya AstraZeneca nadhani itakuwa vigumu kwangu kuipokea lakini, tofauti na hapo kwa sasa nitakuwa ni kuitathmini hali ya ubora wa kila chanjo kabla ya kuipokea,'' alisema mwengine.

Hata hivyo, Waziri wa Afya wa Rwanda Dokta Daniel Ngamije ametupilia mbali wasiwasi wa baadhi ya wananchi hao akisema huo ni mtazamo potofu kwa sababu chanjo hizi zimetolewa kwa mataifa baada ya kuthibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.

Rwanda inaendelea na mazungumzo kwa ajili ya chanjo zaidi

''Mimi niwaombe wananchi kutambua kwamba hizi chanjo ni salama, na zimekaguliwa katika viwango vya kimataifa kiasi kwamba chanjo zote zinazoingia nchini zina uwezo wa kumlinda mtu dhidi ya virusi vya corona,'' alisema Dokta Ngamije.

Waziri Ngamije amesema kwamba Rwanda inaendelea na mazungumzo na pande husika kuagiza chanjo zaidi.

Rwanda yakanusha kukubali majaribio ya dawa ya corona

This browser does not support the audio element.

''Tunatazamia kuleta chanjo nyingine baada ya kuthibitishwa ubora wake, kama vile chanjo ya Johnston na Johnston kutoka Marekani maana tunaendelea na mazungumzo. Kadri chanjo zitakavyopatikana ndivyo tutakavyozidi kuagiza lakini tukizingatia ubora wake na bei yake,'' alisema Dokta Ngamije.

Waziri huyo wa afya pia amesema kwamba kuanzia sasa Rwanda itakuwa ikipokea chanjo za virusi vya corona kila mwezi ambapo wiki ijayo itazipokea chanjo nyingine laki tano kupitia pia mpango huu. Rwanda inatarajia kuagiza jumla ya chanjo milioni saba lengo likiwa ni kuchanja asilimia 60% ya wananchi wake wote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW