1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda yasema ndege ya kivita ya Kongo imekiuka anga yake

25 Januari 2023

Serikali ya Rwanda imesema ndege ya kivita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo imekiuka sheria na kuingia katika anga yake hapo jana, huku mvutano ukizidi kutanuka kati ya majirani hao wawili.

Russland Kampfjet Suchoi Su-25SM
Picha: Erik Romanenko/Tass/imago images

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, amesema ndege ya kivita aina ya Sukhoi 25 kutoka Congo iliingia katika anga yake kwa mara ya tatu, kupitia Rubavu karibu na mji wa Goma na hatua za kujilinda zikachukuliwa, huku akiitaka DRC kuacha kuichokoza Rwanda.

Hata hivyo Congo imekanusha kuwa moja ya ndege zake imeingia katika anga ya Rwanda na kulituhumu moja kwa moja taifa hilo kuishambulia ndege yake na kuliita tukio hilo kama hatua ya kuanzisha vita. Congo imesema Rwanda imeshambulia kwa maksudi ndege hiyo kwa nia ya kusambaratisha juhudi za kuleta amani Mashariki mwa Congo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW