Rwanda yatangaza mwisho wa mlipuko wa kirusi cha Marburg
14 Novemba 2024Matangazo
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa la Afrika CDC, Nsanzimana amesema hakujashuhudiwa visa vyovyote vya maambukizi ya Marburg kwa karibu wiki mbili nchini Rwanda.
Waziri huyo wa afya pia amesema umepita mwezi mmoja bila kuripotiwa kifo chochote kilichotokana na virusi hivyo.
Rwanda: Hakuna maambukizi mapya ya Marburg katika siku za karibuni
Mlipuko wa kirusi cha Marburg uliripotiwa kwanza nchini Rwanda na mnamo mwezi Oktoba chanjo dhidi ya kirusi hicho zikaanza kutolewa. Marburg ni kirusi kilicho katika familia moja na Ebola na kinasambazwa kwa binadamu kupitia popo.