1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaRwanda

Rwanda yathibitisha maambukizi ya virusi vya Marburg

28 Septemba 2024

Wizara ya afya ya Rwanda imethibitisha hapo jana maambukizi ya kwanza ya ugonjwa hatari wa Marburg.

Virusi vya Marburg
Virusi vya MarburgPicha: Science Photo Library/IMAGO

Hata hivyo wizara hiyo haikutoa idadi ya walioambukizwa virusi hivyo ambavyo vinaweza kusababisha kifo.

Mamlaka zimesema zinachunguza ili kufahamu kitovu cha maambukizi ya ugonjwa huo ambao unafanana na Ebola, na kusisitiza kuwa wagonjwa wanaendelea kupatiwa matibabu.

Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa, kutapika, kuumwa na tumbo, misuli na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili. Nchi jirani ya Tanzania ilikuwa na kesi za Marburg mwaka jana huku Uganda ikiripoti visa vya maambukizi mwaka 2017.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW