1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda yatishia kuondoa wanajeshi wake Msumbiji

Saleh Mwanamilongo
15 Machi 2026

Rwanda imetishia kuviondoa vikosi vyake vya kupambana na ugaidi nchini Msumbiji ikiwa wafadhili wa kimataifa hawataendelea kutoa fedha za kudumu.

Kigali, Rwanda | Wanajeshi wa Rwanda wakielekea Msumbiji
Vikwazo hivyo vilionyesha mabadiliko yanayoendelea katika sera ya serikali ya Marekani kuelekea Rwanda, ambayo kwa miaka mingi imeepuka kulaumiwa kimataifa kutokana na madai ya ushiriki wake wa kijeshi katika eneo la jirani yake KongoPicha: Simon Wohlfahrt/AFP

Waziri wa Rwanda wa  Mambo ya Nje, Olivier Nduhungirehe amesema vikosi vya Rwanda vinakabiliwa na mashaka, lawama na ukosoaji kutoka nchi ambazo zinafaidika na uwepo wao Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji

"Tukishashindwa kupata ufadhili endelevu, Rwanda itaviondoa vikosi vyake," amesema Nduhungirehe.

Wiki iliyopita, Marekani ilizuwia viza kwa baadhi ya maafisa wa Rwanda kwa kile Washington imesema "kuchochea mzozo mashariki mwa Kongo," ikiongeza shinikizo baada ya vikwazo vya kijeshi.

Vikosi vya Rwanda vinasaidia kupambana na wanamgambo wa Dola la Kiislamu nchini Msumbiji, waliyoanzisha mashambulizi makali mwaka 2017.

Operesheni hiyo imewaletea usalama wakaazi na kuruhusu miradi ya maendeleo kuendelea, ikiwa ni pamoja na mradi wa gesi asilia wa kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies.

Serikali ya Rwanda inasema jitihada zake za kijeshi zinapaswa kuthaminiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW