AfyaRwanda
Rwanda yazuia matumizi ya dawa inayoshukiwa kuwa na sumu
15 Aprili 2024Matangazo
Hatua hiyo ya tahadhari imechukuliwa baada ya Nigeria kusema vipimo vya maabara ya dawa hiyo ya maji vilionyesha kiwango kikubwa cha aina ya kemikali ya diethylene glycol inayohusishwa na vifo vya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.
Rwanda imeungana na Kenya, Afrika Kusini na Nigeria kurejesha dawa hizo zinazotumika kutibu kikohozi, homa kali na mzio kwa watoto.
Dawa zilizorejeshwa zilitengenezwa na kampuni ya J&J nchini Afrika Kusini mwezi Mei mwaka 2021 kabla ya kuuzwa kwa kampuni ya Kenvue ambayo sasa inamiliki chapa ya Benylin Paediatric syrup. Kenvue imesema inafanya uchunguzi wake na kufanya kazi na taasisi za afya kuangalia hatua inayoweza kuchukua.