Rwanda,Boko Haram na Uchumi wa Afrika Magazetini
26 Mei 2017Tunaanzia na gazeti la mjini Berlin die Tageszeitung linalochambua umuhimu wa kuripoti kuhusu mauwaji ya halaiki. Gazeti limechukua mfano wa mauwaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 Linakumbusha shida zilizokuwepo wakati ule kupata habari za kuaminika kuhusu yaliyotokea. "Mauwaji ya halaiki yalipoanza, vyombo vya habari vya kimataifa vilikuwa havikujitayarisha, na taz pia.
Lakini nini hasa kimetokea linajiuliza gazeti la die Tageszeitung. Gazeti limenukuu kilichoandikwa miezi michache kabla na ripota wake mjini Kigali aliyezungumzia hali ya wasi wasi iliyokuwa imetanda wakati ule nchini Rwanda, baada ya kushindwa kutekelezwa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya rais wa wakati ule wa kihutu na wanamgambo wa kitutsi wa RPF yaliyofikiwa mwaka 1993. Hali kama hiyo ilitanda pia katika nchi jirani ya Burundi ambako njama ya mapinduzi ya wanajeshi wa kitutsi dhidi ya rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasi, Oktoba mwaka 1993 ilipelekea damu kumwagika. Nini hasa kimetokea, maafisa wa serikali walionekana kutojua chochote sawa na waandishsi habari ambao pia hawana walichokuwa wakikijua.
Umuhimu wa kutafuta ukweli wa mambo na kuutaja kama ulivyo
Miaka 23 baada ya mauwaji ya halaiki ya Rwanda, bado suala hilo halijapata jibu."Nchini Rwanda sawa na kwengineko, kuna waliokuwa wahalifu na wahanga, kuna wanaobeba jukumu na waliotoa amri na wale wanaotekeleza amri hizo." limeandika gazeti la die Tageszeitung katoka toleo lake la April 13 lililokuwa na kichwa cha maneno "Rwanda hakujatokea janga la kimaumbile. "Hoja hiyo haitokani na ukosefu wa busara au nidhamu ya uandishi, bali inatokana na umuhimu wa kutafuta ukweli wa mambo na kuutaja kama ulivyo.
Maradhi ya kupooza Nigeria
Boko Haram ni sawa na maradhi" linaandeika gazeti la der Freitag linalozungumzia mapambano yanayoendeshwa na serikali ya Nigeria kaskazini mwa nchi hiyo dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa Boko Haram kwa upande mmoja na pia dhidi ya kurejea upya maradhi ya kupooza viungo vya mwili vya watoto. Gazeti linazungumzia jinsi mashirika ya wanawake wanavyojitolea kuwatanabahisha watu katika jimbo la Kano wakubali watoto wao wenye umri wa chini ya miaka mitano wachanjwe ilikujikinga na maradhi hao.
Kwa sasa kuna nchi tatu tu ambako maradhi hayo ya kupooza yanakutikana, Nigeria, Afghanistan na Pakistan. Nigeria ilikuwa itangazwe kuwa nchi iliyoyashinda nguvu maradhi hayo mwaka huu, lakini virusi vikarejea tena. Na sio kwasababu juhudi haiendelezwi. Juhudi zinazoendeshwa na Nigeria kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia watoto-UNICEF zinasifiwa na kutajwa kuwa ni za kijasiri. Lakini tatizo linasabaishwa na wanamgambo wa itikadi kali ya dini ya kiislam Boko Haram.
Gazeti la der Freitag linasema magaidi hao wanaodhibiti baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Nigeria, hawaruhusu watoto wanaoishi katika maeneo hayo kuchanjwa dhidi ya maradhi ya kupooza. Na kuna uwezekano pia wa kuenezwa maradhi hayo katika maeneo mwengine, pale wakaazi wa maeneo yanaodhibitiwa na Boko Haram wanapotoroka. Der Freitag limezungumzia kadhia mbili za maradhi hao zilizogunduliwa Maiduguri-mji mkuu wa jimbo la Borno.
Uchumi wa Afrika unaanza kuimarika
Ripoti yetu ya mwisho inazungumzia matumaini ya ukuaji wa kiuchumi barani Afrika. Lilikuwa gazeti la Frankfurter Allgemeine lililozungumzia matumaini hayo. Baada ya ukuaji wa kiuchumi wa asili mia 2.2 mwaka 2016, mwaka huu uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asili mia 3.4 - limeandika Frakfurter Allgemeine lililonukuu ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, ile ya shirika la Ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo-OECD na pia mpango wa Maendeleo wa umoja wa mataifa. Mwaka jana ukuaji wa kiuchumi ulikuwa haba ukilinganishwa na kuongezeka idai ya wananchi kwa namna ambaayo pato la kila mkaazi lilipungua pia. Sababu ya hali hiyo linaandika Frankfurter Allgemeine inatokana na bei hafifu ya mali ghafi katika maoko ya dunia.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/BASIS/PRESSER/ALL/presse
Mhariri: Josephat Charo