Saad al-Hariri ateuliwa tena kuwa waziri mkuu wa Lebanon
22 Oktoba 2020Hariri amepata uungwaji mkono wa wabunge walio wengi katika mashauriano na Aoun. Anakabiliwa na changamoto kubwa kushawishi siasa za kugawana madaraka za Lebanon, na kukubaliana juu ya baraza, ambalo linapaswa kushughulikia orodha inaoyoongezeka ya masaibu, yakiwemo mgogoro wa mabenki, mporomoko wa sarafu ya nchi, umaskini unaoongezeka na mzigo wa madeni ya taifa.
Changamoto za serikali mpya
Serikali mpya pia itapaswa kupambana na ongezeko la ugonjwa wa Covid-19, na athari za mlipuko mkubwa wa Agosti katika bandari ya Beirut, ambao ulisabisha vifo vya karibu watu 200 na uharibifu wa mamilioni ya dola. Serikali ya mwisho ya Hariri iliangushwa karibu mwaka mmoja uliopita, kufuatia maandamano ya hasira dhidi ya watawala wa Lebanon. Hariri ameungwa mkono na wabunge wa chama chake cha Future, chama cha Kishia cha Amal, chama cha mwanasiasa wa Druze Walid Jumbltt na vyama vingine vidogo. Kundi la kishia la Hezbollah lilisema halitateua mgombea, lakini litashiriki kuwezesha mchakato.