Katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan na Kwaresma, baadhi ya watu hupata kiungulia licha ya kutokula kwa muda mrefu, kwa sababu ya mchanganyiko wa mabadiliko ya ratiba ya kula, aina ya vyakula vinavyoliwa wakati wa kufuturu, na mienendo ya mwili wakati wa njaa huathiri mfumo wa mmeng’enyo. Hali hii inaonekana zaidi kwa watu wenye historia ya kiungulia, lakini inaweza kumpata mtu yeyote.