1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SADC yaondowa wanajeshi wake Mashariki mwa Kongo

13 Machi 2025

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kanda ya Kusini mwa Afrika, SADC imeamua kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kikosi cha kijeshi cha SADC
Kikosi cha kijeshi cha SADCPicha: DW

Uamuzi wa jumuiya hiyo ya wanachama 16 umepitishwa kwenye mkutano wa kilele, uliokuwa ukijadili juu ya mgogoro huo wa mashariki mwa Kongo,ambao umeshuhudiwa kwa karibu miongo mitatu, ukihusisha machafuko na mauaji ya mamilioni ya watu.

Soma pia:Viongozi wa jumuiya ya SADC kujadili mgogoro wa Kongo

Baada ya mazungumzo  yaliyofanyika kwa njia ya mtandao,taarifa ya viongozi wa SADC iliyotolewa ilisema, wamekubaliana kufuta mamlaka ya kikosi cha SAMIDRC ya kuendelea kubakia nchini Kongo na kutowa maelekezo ya kuanza kwa awamu mpango wa kuondoka kwa wanajeshi wa kikosi hicho.

Zaidi ya wanajeshi 12 wa kikosi hicho wameuwawa katika mgogoro wa mashariki mwa Kongo tangua mwezi Januari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW