1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SADC yarefusha muda wa jeshi lake Kongo

21 Novemba 2024

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC imerefusha kwa mwaka mmoja muda wa kikosi chake cha kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mashariki ya Kongo
Jeshi la SADC linaisaidia serikali ya Kongo kupigana na makundi ya waasiPicha: AUBIN MUKONI/AFP

Jeshi la SADC linaisaidia serikali ya Kongo kupigana na makundi ya waasi. Ujumbe huo wa kijeshi ulipelekwa Kongo mnamo Desemba 2023 kuhudumu kwa mwaka mmoja.

Soma pia: Vikosi vya SADC vyafanya msako dhidi ya M23

Taarifa iliyotolewa baada ya viongozi wa kikanda kukutana katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare ilielezea wasiwasi wa usalama na hali ya kibinaadamu nchini Kongo na ikasisitiza uungwaji mkono wa jumuiya hiyo kwa serikali. Kongo ni moja ya mataifa 16 wanachama wa SADC.

Wakati huo huo, viongozi wa vyama vikuu vya upinzani Kongo wametoa wito wa kufanyika maandamano ya kitaifa dhidi ya mipango ya Rais Felix Tshisekedi kuandika katiba mpya. Viongozi hao ni pamoja na Rais wa zamani Joseph Kabila na wagombea urais wa zamani Martin Fayulu na Moise Katumbi.