1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sadio Mane asema wako katika kundi gumu AFCON

10 Januari 2024

Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal, Simba wa Teranga, Sadio Mane amesema kundi gumu linawasubiri mabingwa hao watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika AFCON.

Mandalizi ya AFCON | Sadio Mane
Sadio Mane aelezea hofu dhidi ya washindani wa kundi la timu yake AFCON.Picha: REUTERS

Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal, Simba wa Teranga, Sadio Mane amesema kundi gumu linawasubiri mabingwa hao watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika AFCON wakati watakakwaana na Gambia, Cameroon na Guinea kwenye mechi za makundi.

Mane amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa ngumu sana na hawathubutu kuwadharau wapinzani wao.

Soma pia:Mataifa ya Afrika Mashariki yaandika historia AFCON 

Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa soka Afrika amewaambia waandishi habari kwamba hakuna mechi hata moja itakayokuwa rahisi ktika kundi lao la C lakini wana uwezo na ari ya kusonga mbele kufikia duru ya mtoano huku michuano ya AFCON ikitarajiwa kuanza Jumamosi wiki hii nchini Ivory Coast.

Senegal iliipiku Cameroon miaka 34 iliyopita katika mechi ya makundi nchini Algeria wakati zilipokutana kwa mara ya kwanza katika mashindano ya kombe la matafa ya Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW