1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za ndege kurejea Ulaya?

13 Mei 2020

Kuna uwezekano sasa kwamba safari za ndege zikarejea baada ya mataifa ya Ulaya kuanza mkakati wa kuzirejesha kufuatia kufungwa katika mkakati wa kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

USA | Donald Trump | Maskenpflicht für Mitarbeiter im Weißen Haus
Picha: picture-alliance/Pool via CNP/O. Contreras

Huku mataifa kadhaa yakianza kuzifunguwa chumi zao baada ya miezi kadhaa ya kuzifunga kutokana na janga la virusi vya corona, baraza la Wawakilishi la Marekani limetangaza kitita cha dola trilioni tatu kwa ajili ya hatua hiyo na hapa Ulaya mipango ya kufunguliwa mipaka na kurejeshwa kwa safari za ndege ikianza. 

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amezinduwa mpango huo wa uokozi wenye thamani ya dola trilioni tatu, ambapo trilioni moja kati yake zitakwenda kwa serikali za majimbo na miji, malipo ya majanga kwa wahudumu muhimu na awamu mpya ya fedha taslim kwa watu mmoja mmoja, msisitizo ukiwekwa hasa kwa wafanyakazi wa huduma za afya.

"Lazima tuwe na huruma kwa mashujaa wetu, wahudumu wa afya, kwa jinsi wanavyochoka na wanavyofadhaika wakati wakitimiza wajibu wao. Na kwa hilo, wanaweza kupoteza ajira zao kwa hali ya uchumi ilivyo. Pia tunapaswa kuzihurumia familia ambazo hazijuwi wapi watakitolea chakula chao na vipi watalipa kodi zao nyumba kwa mwezi ujao."

Baraza hilo la Wawakilishi linatazamiwa kuupigia kura mpango huo keshokutwa Ijumaa, lakini kiongozi wa walio wengi kwenye Baraza la Seneti, Mitch McConnel, amesema hakuna jambo la dharura kiasi hicho, na kwamba baraza la Seneti litangojea hadi baada ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ndipo wazingatie la kufanya.

Ulaya inaanza kufikiria utaratibu wa kurejesha safari za ndegePicha: Imago Images/M. Lorenz

Hapa barani Ulaya, Austria imesema kuwa itafunguwa mpaka wake na Ujerumani mwezi ujao. Shirika la habari la nchi hiyo limeinukuu ofisi ya kansela ikisema kuwa mpaka utafunguliwa kwa ukamilifu mnamo tarehe 15 Juni, lakini masharti ya mipakani yataanza kulegezwa keshokutwa Ijumaa. Hatua kama hiyo pia itachukuliwa kwa mataifa jirani ya Uswisi, Liechtenstein na ya Ulaya Mashariki.

Nayo kampuni kubwa ya utalii barani Ulaya, TUI imesema kuwa huenda ikapunguza idadi kubwa ya wafanyakazi wao wakati ikipambana na hasara iliyopata kutokana na janga la virusi vya korona.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu hapa Ujerumani imesema hiyo hivi leo kwamba itaanza shughuli zake tena hivi karibuni, kwa kupeleka watalii kwenye hoteli za fukwe za Ujerumani. TUI inalazimika kupunguza wafanyakazi wake hata baada ya kupokea kitita cha mkopo wa euro bilioni 1.8 kupambana na athari za janga la korona.

Soma Zaidi: Vikwazo vyaanza kulegezwa Ulaya, New York

Mashirika: AFP
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW