1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Safari za ndege zacheleweshwa Marekani

11 Januari 2023

Wakala unaosimamia na kuongoza safari za ndege za shirikisho nchini Marekani FAA umetangaza kusitisha safari zote za ndege nchini humo kufuatia hitilafu kwenye mfumo wa kompyuta katika afisi za wakala huo.

Computerpanne: Alle US-Inlandsflüge müssen am Boden bleiben
Picha: Patrick Semansky/AP/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa wavuti unaofuatilia safari za ndege wa FlightAware karibu safari 1,200 za ndege zilichleweshwa kabla saa moja asubuhi hivi leo za kuingia au kutoka Marekani.

Safari nyingi za ndege zimecheleweshwa katika pwani ya mashariki ya Marekani. Wakala huo umesema unafanya juhudi kurekebisha hitilafu katika mfumo wake wa usimamizi wa safari za ndege.

Ndege zote za biashara na jeshi zinatakiwa kuongozwa na mfumo huo katika safari zao. Msemaji wa ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre amesema hakuna ushahidi wa shambulizi la mtandaoni na Rais Joe Biden amefahamishwa kinachoendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW