1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Safari za ndege zatatizika kuelekea Afrika Magharibi

Hawa Bihoga
7 Agosti 2023

Mashirika ya ndege ya Ulaya yameripoti hii leo kuvurugika kwa safari za ndege na kusitisha safari za Afrika baada ya utawala wa kijeshi nchini Niger kufunga anga yake jana Jumapili.

Deutschland, München | Pilotenstreik bei der Lufthansa
Picha: Boris Roessler/picture alliance/dpa

Kuvurugika kwa safari za ndege kunaongeza idadi ya anga za mataifa ya Afrika zinazokabiliwa na hali uvurugaji wa kijiografia, zikiwemo la Libya na Sudan, ambapo ndege zinalazimika kusafiri umbali wa hadi kilomita 1,000 za ziada.

Kampuni ya kufuatilia safari za ndege ya FlightRadar24, imesema katika chapisho la blogu kwamba kufungwa kwa anga ya Nigerkunaongeza pakubwa eneo ambalo ndege nyingi za abiria zinazosafiri kati ya Ulaya na kusini mwa Afrika haziwezi kupita.
Soma pia:Shinikizo lazidi kuongezeka kwa viongozi wa mapinduzi Niger

Shirika la ndege la Ufaransa Air France kwa mfano limesitisha safari za kwenda na kutoka Ougadougou nchini Burkina Faso, na Bamako nchini Mali hadi Agosti 11, huku likitarajia kutumia muda mrefu zaidi wa safari katika kanda ya Afrika Magharibi.

Msemaji wa shirila la ndege la Ujerumani Lufthansa, na Brussels Airlines la Ubelgiji, wamesema mida ya safari inaweza kuongezeka kwa kati ya saa moja na nusu hadi masaa matatu na nusu kwa safari zilizobadilishwa njia.

Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, limesema kwamba limeomba radhi kwa wateja wake walioathiriwa na uvurugaji wa safari zao.

Haya ni matokeo ya mapinduzi ya kijeshi?

Niger ilitangaza kufunga anga yake jana Jumapili kutokana na kile ilichokitaja kuwa kitisho cha uvamizi uliokuwa unaandaliwa katika mataifa mawili ya Afrika ya Kati, huku muda uliotolewa kwa utawala wa kijeshi kumrejesha madarakani rais Bazoum ukifikia mwisho jana Jumapili.

Niger yafunga anga yake huku wasiwasi ukiongezeka baada ya mapinduzi

02:09

This browser does not support the video element.

Akitangaza uamuzi wa kufunga anga hiyo, mwanachama wa Baraza la taifa la ulinzi wa nchi Amadou Abdramane, alisema sababu za kiusalama ndio sababu ya kufunga anga.

"Anga ya Niger imefungwa kwa ndege zote kuanzia leo, Jumapili 6 Agosti 2023, hadi taarifa nyingine."

Alisema na kuongeza kuwajaribio lolote la kukiuka anga ya kitaifa litakabiliwa na jibu la nguvu na la papo hapo.

Msemaji wa ECOWAS amesema hii leo kuwa viongozi wake watakutana tena siku ya Alhamis katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kujadili namna ya kuishughulikia nchi hiyo.

Ujerumani nayo imewaonya watawala wapya kutomdhuru rais alieondolewa madarakani Mohamed Bazoum, na kutishia kuwachukulia hatua kali ikiwemo vikwazo.

Soma pia:Niger yangoja uvamizi wa kijeshi wa ECOWAS

Mali na Burkina Faso, ambazo pia zilisimamishwa uanachama wa ECOWAS baada ya serikali zao kuondolewa kupitia mapinduzi, na zina mpaka na Niger, zimeunga mkono utawala wa kijeshi na kutishia kuchukulia uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Niger kuwa tangazo la vita dhidi yao.

Nchi hizo zimesema zinatuma ujumbe rasmi nchini Niger kuonyesha mshikamano na watawala waliofanya mapinduzi.

Rais Bazoum alikamatwa, kutangazwa kuwa ameondolewa na kisha nafasi yake kuchukuliwa nakiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdourahamene Tchiani, aliesitisha katiba na kuvunja taasisi zote za kikatiba.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW