Katika siku za hivi karibuni, mashambulizi ya pamoja ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran zimeifanya sekta ya usafiri wa anga Mashariki ya Kati kukumbwa na msukosuko mkubwa. Mashirika ya ndege yamelazimika kusimamisha safari, kubadilisha njia au kufuta kabisa safari zilizopangwa, hatua ambayo imeathiri maelfu ya wasafiri wa kimataifa.