1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za ndege zimesitishwa katika uwanja wa Munich

5 Desemba 2023

Shughuli katika uwanja wa ndege wa Munich, Kusini mwa Ujerumani zimesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa ya baridi kali na barafu.

Deutschland München | Schneechaos in Süddeutschland | Münchner Flughafen
Picha: Angelika Warmuth/REUTERS

Msemaji wa uwanja huo mkubwa wa ndege amethibitisha kwamba shughuli za usafiri wa ndege kwa mara nyingine leo asubuhi zimesimamishwa kutokana na kuganda kwa barafu katika barabara za kurusha ndege kufuatia mvua na baridi kali. Hakuna ndege iliyoruhusiwa kuruka wala kutuwa katika uwanja huokuanzia asubuhi na shughuli ya kuongoa barafu itafanyika katika kipindi cha nusu nzima ya siku. Kwa mujibu wa msemaji wa uwanja huo wa ndege, pamoja na zoezi hilo kufanyika, safari nyingi za ndege zitalazimika kufutwa kwa siku nzima leo kutokana na sababu za kiusalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW